Michezo

Roger Federer ang’ara tuzo za Laureus World Sports

Mchezaji tennis raia wa Uswis, Roger Federer ametwaa tuzo mbili za  Laureus World Sports Awards kwa mwaka huu wa 2018 katika sherehe zilizofanyia huko Monaco usiku wa Juamanne ya wiki hii. 

Federer ametwaa tuzo hiyo ya Laureus World Sports Awards katika kipengele cha mchezaji bora wakiume wa mwaka na mchezaji aliyerejea na kufanya vizuri.

Mchezaji huyo ambaye anashikilia nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018 baada ya kutwaa taji lake la 20 la Grand Slam la michuano ya Australia akiwa anatoka katika majeraha yaliyokuwa yakimuandama huku akishindana na Cristiano Ronaldo na Rafael Nadal kwenye kipengele hicho cha Sportsman of the Year.

Kwa upande wa wanawake Serena Williams ametwaa tuzo hiyo ya Sportswoman of the year.

Tuzo hii imejumuisha michezo mbalimbali pamoja na timu kama ilivyo kwa Roger Federer, akiwemo Cristiano Ronaldo  ambaye alikuwa akiwania Laureus World Sportsman, timu ya  Real Madrid ikiwa katika kipengele cha  Laureus World Team of the Year, mchezaji wa PSG, Kylian Mbappé akiwa  Laureus World Breakthrough of the Year , FC Barcelona na Chapecoense wakingia katika kipengele cha Laureus World Comeback of the Year Award.

Tuzo hizi za Laureus World Sports Awards zina husu wachezaji mmoja mmoja na timu huku zikianzishwa mwaka 1999 na sherehe zake za kwanza zikifanyika mwaka 2000 huko Monte Carlo wakati rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiwa ndiyo mtoa hutuba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents