Michezo

Roger Federer ayaaga mashindano ya US Open

Mcheza tenis raia wa Argentina, Juan Martin del Potro amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani ‘US Open’ baada ya kumtoa Roger Federer.

Mchezaji tenis, Roger Federer (kushoto) akimaliza mchezo na Juan Martin del Potro (kulia)

Del Potro amemtoa mchezaji huyo bora anaeshikilia nafasi ya tatu katika viwango vya ubora ulimwenguni kwa jumla ya seti 7-5 3-6 7-6 (10-8) 6-4 katika mashindano yanayo endelea huko New York nchini Marekani.

Mchezaji huyo wa Argentina sasa anatarajia kukutana na mhispania, Rafael Nadal anaeshikilia nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa mchezo huo ambaye alitinga hatua hiyo baada ya kumtoa kijana mdogo raia wa Urusi, Andrey Rublev.

Ushindi wa Del Potro unafanya wachezaji hawa wawili, Federer na Nadal kushindwa kukutana katika michuano hii ya US Open hivyo pengine mpaka mwakani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents