Michezo

Roger Federer na Del Potro wawa gumzo michuano ya Miami Open

Baada ya wachezaji tennis, Roger Federer na Juan Martin del Potro kutangazwa kushiriki michuano ya wazi ya Miami (Miami Open) mwishoni mwa juma hili kumezuka gumzo kubwa miongoni mwamashabiki wa mchezo huo.

Gumzo hilo linakuja kufuatia wawili hao, Federer na Del Potro kukutana katika mchezo wa fainali ya michuano ya WTA Indian Wells juma lililopita na Muargentina huyo kuibuka na ubingwa mbele ya mchezaji tennis namba moja katika viwango vya ubora duniani Federer.

Del Potro bingwa mpya wa michuano ya Indian Wells

Federer ataingia kwenye michuano hiyo ya Miami Open kwa tahadhari kubwa ili kuhakikisha anatetea ubingwa wake aliyoutwaa mwaka uliyopita lakini pia kunatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi baada ya mpinzani wake wa WTA Indian Wells, Del Potro kuwemo.

Federer akisherehekea ubingwa wake wa Miami Open mwaka jana

Katika mfululizo wa kukosekana kwa wachezaji, Rafael Nadal na Andy Murray pamoja na Novak Djokovic kufuatia majeraha waliyokuwa nayo kunamfanya bingwa Indian Wells, Del Potro kung’ara uwanjani.

Federer atashuka dimbani siku ya Jumamosi katika mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya atakaye fuzu kabla ya kukabilia na Spaniard Fernando Verdasco katika mzunguko wa tatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents