Michezo

Roger Federer: Sitoshiriki mashindano ya wazi ya Ufaransa ‘ French Open’

Mcheza Tenisi anaeshika nafasi ya 5 katika viwango vya ubora Ulimwenguni na mshindi wa mashindano ya wazi ya Ufarasa ya mwaka 2009, Roger Federer , ametangaza hatoshiriki mashindano ya safari hii ya wazi ya Ufaransa {French Open}.


Mcheza Tenisi raia wa Uswisi,Roger Federer

Roger Federer, ametangaza kutoshiriki ili apate muda wa kujiimarisha pamoja kufanya maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Wimbledon. Legendari huyo raia wa Uswiss ambaye hakushiriki mashindano ya 18 ya wazi ya Australia ya mwezi Januari baada ya kutokuwa katika mchezo huo kwa miezi 6 kutokana na kupata majeraha Mei 28 mwaka jana.


Mcheza Tenisi raia wa Uswisi,Roger Federer

Federer,aliweka barua katika tovuti yake siku ya Jumatatu ikielezea kutoshiriki na anajiskia vibaya kwake kukosa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa, “Kwa bahati mbaya sitoshiriki mashindano ya wazi ya Ufaransa” , Alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35.

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa juhudi kubwa sana, ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja, katika kipindi cha mwezi uliopita ili niweze kujaribu kucheza na kuwa katika chama cha wachezaji wa Tenisi wa kulipwa Ulimwenguni {ATP World Tour} kwa miaka mingi ijayo,” Alisema Federer.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents