Burudani

Roma achambua mistari ya ngoma ‘Zimbabwe’

Msanii wa hip hop Bongo, Roma amefafanua moja ya mistari inayopatikana katika ngoma yake mpya ‘Zimbabwe’ ambayo kwa sasa ni moja ngoma zinazofanya vizuri zaidi kwa hapa Bongo.

Hata hivyo Roma amekiri kuwa wimbo huo umekuwa na tafsiri nyingi sana mtaani kwani kila mtu ana mtazamo wake na kueleza kuwa ni kitu cha kawaida pindi msanii anaposhirikisha jamii katika muziki.

Na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili, Godbless imetimia injili nilioitabiri.

Hiyo ni mistari inayopatikana katika ngoma hiyo katika verse ya pili mwishoni ambapo ameeleza kuwa ni kama shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanikisha kupatikana kwake wakati alipopatwa na mkasa wa kutekwa.

“Wife aliungana na wasanii wengi kipindi cha tatizo na katika jitihada za kunitafuta walifanikiwa kwenda kwa Mkuu wa Mkoa na wakaomba msaada na Mkuu akawapokea vizuri akawasaidia katika kiwango kikubwa hadi tukaja tukakaa sawa, niliadithiwa kwa sababu mimi sikuwepo,” Roma ameiambia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.

“Lakini kibinadamu kutokana na kile kilichofanyika, inabidi urudi utoe shukrani na tukalifanya hivyo tukaenda kutoa pongezi kwamba  tulifanya hiki na hiki na tukaja Mkuu wa Mkoa tunakushuru na sasa hivi maisha yanaendelea,” amesema Roma.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents