Burudani

Roma alilia nafasi ya wasanii wenye vipaji

Kuna majina mengi makubwa yanafahamika kwenye muziki, lakini kwa wasanii wenye vipaji kati yao ni wachache. Roma ameshauri wasanii wenye vipaji wapewe nafasi kubwa zaidi kwenye industry.

Rapper amesema kwamba kwa kufanya hivyo, kutakuja kusaidia baadae kwa kuwa madhara ya kutokufanya haya, halitaonekana sasa hivi ila ni baada ya kupita miaka kadhaa ndio litaonekana.

“Tusi ignore vipaji asilia, yule mwenye kipaji tumpe nafasi kwa sasa hatutaliona hilo ila baada ya miaka mitano au 10 mbele tunaweza kuona madhara yake kwa sababu tutakuwa tumeshaaanguka tayari na tunashindwa kukumbuka wapi tulijikwaa,” amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.

“Hata katika media house tunakosa mabalozi wanaosimamia vipaji ili tupate balance ya hiki kitu kwenye media house kuwe na mabalozi ambapo watajua msanii anatengeneza kazi nzuri, nimpe support na nimuangalie in a positive way,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents