Roma asema maneno ya mwisho aliyoambiwa na Sajuki, ‘Sitamaliza siku 7 ntakuwa nimeaga dunia’

Roma 22

Kupitia ukurasa wake wa Facebook rapper wa 2030, Roma Mkatoliki amesimulia maneno ya mwisho aliyoambiwa na marehemu Sajuki.

NINACHOKUMBUKA SHOW YA MWISHO ARUSHA YA KUMCHANGIA SAJUKI!!TUKIWA CHUMBANI KWAKE MIMI, WASTARA, DJ CHOKA, YUSUPH MLELA NA WENGINEO, SAJUKI ALIMSHIKA MLELA MKONO HUKU AKIMTAZAMA KWA HUDHUNI NA AKAMWABIA
“SITAMALIZA SIKU 7 NITAKUWA NIMEIAGA DUNIA”ILIKUWA HARD TYM SANA KWETU NA WENGI TULILENGWA NA MACHOZI KWA KAULI ILE!!

LEO LIMETIMIA LILE NENO…oooh god mfutie dhambi zake na muepushe na adhabu za huko!! nasisi tupate somo kuwa maisha yanaweza yakabadilika within a second!!Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa amani!!! poleni sana marafiki wenzangu.

Wakati huo huo mazishi ya Sajuki yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents