Burudani

Roma atoa majibu 10 ya maswali ambayo huulizwa na mashabiki wake mara kwa mara

Mara nyingi mashabiki wa muziki au filamu huwa na maswali mengi kuhusiana na wasanii wanaowapenda lakini huwa hawapati nafasi za kuwauliza tofauti na wawapo kwenye vipindi vya radio ambapo pia nafasi huwa ni ndogo ya kupiga simu so hubaki na maswali yao bila kuwa na majibu.

Roma

Rapper wa ‘2030’ Roma Mkatoliki ni mmoja kati ya wasanii wenye mahusiano mazuri na mashabiki wao katika mitandao ya kijamii hususan facebook. Kuthibitisha hilo muda mfupi uliopita ameandika majibu 10 ya maswali ambayo huulizwa na mashabiki wengi wa facebook.

Haya ndio majibu ya maswali hayo kama alivyoyajibu katika akaunti yake ya facebook.

1. R.O.M.A ni muumini wa dini ya kikristo(R.C) aliyezisoma sakramenti zote 7 na kupokea ya ubatizo/ekaristi takatifu na hata kipaimara…nangoja NDOA!!

2. Ile sauti mnayosikiaga ikisema TONGWE RECORDS BEIB siyo ya ROMA ni JOSLIN!!ambae naye ni miongoni mwa wasanii walio chini ya tongwe!! plus KAMIKAZE/JOS MTAMBO/DOMO KAYA/SAIGON/NORMAN WA BSS/

3. Kuna J. MURDER ambae ndiye CEO wa tongwe records, na kuna J.RYDER ambaye ndiye anagonga midundo ya TONGWE RECORDS. watu wawili tofauti!!

4. Tongwe records ni studio zilizopo daresalaam mitaa ya masaki/ dakika kama 3 tu kutokea coco beach!! na haipo kigamboni kama wengi wanavyodhani!! lakini tanga kuna kijiji kinaitwa TONGWE na ndicho kijiji ama himaya ya J. MURDER!! ambaye ndiye huyo mmiliki!!

5. Sijawahi kufungwa wala kwenda jela/ sijawahi kuitwa ikulu/ nyimbo zangu za awali tanzania/ mr president ndiyo zilipigwa stop kupigwa ktk baadhi ya vituo vya radio, kwa sababu zao binafsi!!

6. Mimi kwetu ni TANGA nimezaliwa na kukulia na kusoma na kuanza muziki TANGA/ kiasili ni mpare(SAME KILIMANJARO) na mama ni mchaga!! kikabila utani unaruhusiwa, mpare mtani wake mchaga, ndiyo maana mchaga siku zote namuona ni mtani wangu(MSIPANIKI)!! nadumisha mila ya utani!!

7. Katika face book account yangu niitumiayo ni hii ya Roma Tongwe na pia kuna page yangu inaitwa R.O.M.A na kuna group inaitwa ONGEA NA ROMA baaaasiii!! lakini kuna wana tu kwa mapenzi yao ama kwa uduanzi wao huamua na wamefungua akaunti kibao wakijiita Roma mkatoliki/Roma mtanzania/Roma Tanga/ na zingine, tena ukizipitia jamaa wana marafiki wengi kuliko hata mimi, na wanazi-run kama mimi yaani nao wanapost kabisa ETI OYAA MOROGORO HERE I COME…hahahahahha bongo bana!!

8. Aliyeimba chorus ya 2030 ni mtoto wa rafiki yangu anaitwa STORY, ni mtoto wa miaka 7hiviii!! lakini chorus ile iliimbwa miaka ya 90 naa zamani sana na binti mmoja ambaye kwa sasa amekuwa sana!!!

9. Nilianzisha mtindo wakuuza nyimbo zangu on-line(BUT LOKO) na kama trial nilianza na 2030(tsh 3000/=), ilikuwa ni nyimbo inayohitajika sana na wenye mapenzi na kuujua umuhimu wa kazi ya sanaa walinunua(sio woote) ila kati ya marafiki 5000 wa fb walinunua takribani watu 500 tu!! hadi sasa siwezi na sijawahi mtumia mtu nyimbo yangu akiniomba for free!! it z for sale!! 3000 per track!! otherws tumia indirect ways!!

10. Natoa ngoma 1 kwa mwaka!! tokea naanza game hii, ndiyo utaratibu niliojiwekea, najaribu kufanya LIVING SONGS!!(nyimbo zinazodumu/zinazoishi, kana kwamba ukisikia jogoo la tanzania linawika sasa uamke kwenye kiti chako turuke ruke!!) wapo artist ambao ndani ya miezi 6 wanatoa ngoma hata 4, na zinaweza feli zote, ama zikafaulu zote!! ni sawa kwa upande wao!!ndio njia waliyoichagua!! So toka tanzania 2008 hadi 2030 iliyotoka december 29 2012 siku moja kabla ya 2013!! ipo hivo!!
kwahiyo nadaiwa ngoma mpya mwaka huu!! na SOON ZITATOKA VIDEO 2 ZA ROMA!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents