Burudani

Roma Mkatoliki kuvunja ukimya kwa kuachia video 2 kwa mpigo ikiwemo ya 2030

Mwana Hip Hop, Roma Mkatoliki anatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia video mbili. Moja ni ya wimbo wake alioutoa mwaka jana nyingine ni ya wimbo mpya.

ROM

Roma amesema ameamua kufanya hivyo kama njia ya kuwapoza mashabiki wake aliowaangusha kwa kushindwa kutoa video ya hit yake Mathematics. Amesema alikuwa ameshalipia kufanya video hiyo lakini muongozaji kutingwa na kazi nyingi na hivyo kuichelewesha sababu iliyomfanya rapper huyo aweke kabatini tu kwakuwa ilikuwa imekaa muda muda mrefu sana.

“Tulichojipanga Roma na Tongwe team mzima tufanye video mbili au tatu inawezekana tukatoa video ya 2030 na nyingine mbili mpya na pia video ya Mathematics tulifanya lakini producer alitucheweshea kuturudishia kwahiyo ushauri wa watu wakasema tuiache tufanye kama kumbukumbu,” Roma aliambia Bongo5.

Kutokana na ucheleweshaji wa kazi yake, Roma ameamua kumtafuta director ambaye hajulikani ili mradi afanye kazi nzuri.

“Sijajua kuna matatizo gani kwa kampuni ambayo tuliichagua walikuwa na kazi nyingi, sio kwenye video hata kwenye audio napenda kushauriana mawazo yangu yapewe kipaumbele lakini sijajua tunapishana mawazo na makampuni makubwa kwasababu hawataki kushauriwa. Yeye umuachie kazi yako siku ya siku anakupa cd yako kama amekosea ukimwambia kuna vipande sivitaki au viongezwe anaweza akakujibu vibaya. Kwa sasa tutatafuta kampuni hata iwe ndogo ilimradi itafanya vitu ambavyo nahitaji vifanyike. Unaweza ukamshauri twende Tanga kuna location Nzuri mkaenda lakini sasa wengine ukiwashauri wanaweza kukujibu vibaya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents