Tupo Nawe

Roma na Stamina wamejifungia wenyewe, wanatafuta kiki – BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limekanusa taarifa ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii kwamba wimbo mpya ‘Parapanda’ wa Roma na Stamina umefungiwa.

Taarifa hizo zilianza kuzagaa mara baada ya wawili hao kuitwa na Baraza hilo kwaajili ya kikao cha kujadiliana mambo mbalimbali kusuhu kanuni mpya za baraza hilo zilizotangazwa mapema jana.

Muda mchache baada ya kikao hicho Roma na Stamina alionekana wakilalamika kupitia mitandao ya kijamii kwamba waliitwa kwaajili ya wimbo wao mpya huku wakidai umeonekana una matatizo.

Mapema jana Katibu wa Baraza la Sanaa, Godfrey Mngereza, aliimbia Bongo5 kwamba wawili hao hawakuijwa kwaajili ya wimbo wao.

Akizungumza na mtandao wa Mwananchi Digital, Mngereza alisema “Labda kama wameamua kujifungia wenyewe ili kuufanya wimbo wao ujulikane na watu, lakini sisi hata hatujauona na kuupitia kama taratibu zetu zinavyotaka na mnajua tukifungia wimbo huwa tunatangaza sasa labda Roma awaonyeshe wapi tumesema hivyo,” amesema Mngereza.

Hata hivyo, katibu huyo alikiri kuwa jana wasanii hao wawili kufika katika ofisi za Basata kwa ajili ya kushiriki jukwaa la wasanii ambalo hufanyika kila siku ya Jumatatu katika ukumbi wao uliopo Ilala Gereji huku mada kuu kwa siku hiyo ilikuwa kuhusu kanuni mpya za sanaa zilizoanza kutumika Julai mwaka huu.

Katika jukwaa hilo anasema mmoja wa waandishi aliuliza swali kuhusu matumizi ya picha za waasisi wa mbalimbali wa nchi hii katika sanaa, ambapo Mngereza anadai alimjibu kuwa msanii anapaswa kupata kibali kutoka kwa familia au Serikali.

“Huenda majibu haya labda ndiyo yalimfanya Roma akaondoka pale na tafsiri yake na kuandika hicho alichokiandika, lakini kiukweli hatujamfungia wala kumuita kumuhoji kuhusiana na wimbo hiyo,” amesema Katibu huyo.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW