Michezo

Ronaldinho aachiwa huru na kutoka kizuizini nchini Paraguay

Nyota wa zamani wa Brazil ,Ronaldinho Gaucho ametoka kizuizini alipokuwa anashikiliwa kwa zaidi ya miezi 5 baada ya Mahakama moja nchini Paraguay  kumuhukumu adhabu hiyo kutokana na madai ya hati bandia ya kusafiria.

Ronaldinho Gaucho akiwa mahakamani nchini Paraguay .

Gaucho ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora Dunia na FIFA ,ni mmoja ya wachezaji waliofanya makubwa katika soka la dunia, akitwaa tuzo mbalimbali ikiwemo kombe la dunia mwaka 2002 akiwa mchezaji kinda kabisa nyakati hizo

Staa huyo wa zamani wa vilabu vya PSG,Barcelona na hata AC Milan,likuwa anashikiliwa na mamlaka  za usalama za Paraguay pamoja na kaka yake ,Roberto de Asas ambaye anatambulika kama meneja wa nyota huyu wa zamani .

Nje ya soka Gaucho anatajwa kama mchezaji anayependa sana anasa na maisha ya ufahari yaliyochangia kutofanikiwa zaidi katika soka  na hata sakata hili la kuingia nchini Paraguay kwa hati ya bandia inaelezwa kuwa walikuwa wanakwenda katika uzinduzi wa moja ya kumbi za starehe ya usiku maarufu kama Cassino.

https://www.youtube.com/watch?v=Hx3d4Gb1kk0

 

https://www.youtube.com/watch?v=O0TTas2Pyw0

https://www.youtube.com/watch?v=pPh8nS0QhPs

https://www.youtube.com/watch?v=O0TTas2Pyw0

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents