Michezo

Ronaldo adai hana nia ya kujiunga na klabu ya David Beckham, United na Liver vitani kwa kinda huyu wa miaka 19

Cristiano Ronaldo, 35, amesema kuwa anayofuraha ya kutosha ndani ya kikosi cha Juventus na wala hana nia ya kujiunga na klabu ya Inter Miami inayomilikiwa na aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, David Beckham. (Sky Sports)

Cristiano RonaldoCristiano Ronaldo, 35, amesema anafurahia kuwa Juventus na kwamba hana mpango wa kuondoka klabu hiyo

Hayo yamejiri mara baada ya mmiliki wa klabu hiyo ya Inter Miami, David Beckham kuthibitisha nia yake ya kutaka kuwasajili wafalme wa soka duniani, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho 19, hana mawazo kuhusiana na hatma yake ya baadae licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kuenda Manchester United ama Liverpool. (Mail)

Jadon Sancho

Tottenham wanajiandaa kumsaka kipa wa Watford Ben Foster, 36, ambaye mkataba wake Vicarage Road unamalizika msimu huu wa joto. (Sun)

Spurs pia wanataka kuikosesha Roma nafasi ya kumpata Chris Smalling kutoka Manchester United kwani wana mpango wa kumpatia mkataba wa kudumu.

Beki huyo wa England, 30, kwa sasa yuko katika klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Calciomercato, in Italian)Chris SmallingSpurs kuikosesha Roma nafasi ya kumpata Chris Smalling

United wanapigiwa upatu kumsajili beki wa Napoli, Kalidou Koulibaly. Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye miaka 26, pia anawaniwa na Real Madrid na Paris St-Germain. (Express, via Corriere dello Sport)

United pia wanamfuatilia beki wa Stoke City Nathan Collins, Kiungo huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland aliye na umri wa chini ya miaka 21, amecheza mara 12 katika timu ya kwanza ya Potters. (Sun)

Dries Mertens ,31, anayelengwa na Chelsea anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu ya Napoli. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji inakamilika msimu huu wa joto. (Sun)Kalidou KoulibalyUnited wanapigiwa upatu kumsajili beki wa Napoli Kalidou Koulibaly

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta huenda akapewe fedha kidogo ya za kununua wachezaji msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Champions League msimu ujao licha ya tetesi kuibuka kuhusu hali ngumu ya kifedha inayokumba klabu hiyo. (Goal)

Afisa mkuu mtendaji wa Inter Milan Giuseppe Marotta anahofia msimu wa ligi kuu ya Italia Serie A huenda usimaliziki ikiwa hawatapata suluhisho janga la kiafya la coronavirus. (Mail).

Tetesi Bora Jumapili

 

Barcelona inamnyemelea mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30 ambaye mkataba wake unamlizika mwisho wa simu ujao. (Sunday Express)

Manchester United wako tayari kutoa kima cha £150,000 kwa wiki kwa nahodha wa Aston Villa Jack Grealish ili kuwa Old Trafford katika msimu ujao wa uhamisho. (Sun)

Mshamambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland ndiye anayependelewa na Real Madrid wakati inapojiandaa kuongeza mshambuliaji mwengine kwa msimu wa tatu mfululizo.

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, pia yuko kwenye orodha ya Real Madrid na kumaanisha kwamba huenda Liverpool ikapata upinzani wa kumpata mchezaji huyo wa Ujerumani. (Daily Mail)Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, yuko kwenye orodha ya Real MadridMshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, yuko kwenye orodha ya Real Madrid

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ana imani kwamba ataweza kurejea uwanjani kabla ya mwisho wa msimu huu kutokana na jeraha la mgongoni.

Liverpool itakuwa na kibarua cha kuimarisha safu yake ya mashambulizi msimu ujao kwasababu mchezaji wa kimataifa Adam Lallana, 31, na Xherdan Shaqiri, 28, wa Switzerland wote wanatarajiwa kuondoka mwisho mwa msimu. (The Athletic via Express)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents