Michezo

Ronaldo afunguka kilichomhamisha Madrid ‘Ningetaka fedha ningezifata China, sababu ni rais wa Madrid’

Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo amesema kuwa aliihama Real Madrid na kujiunga na miamba hiyo ya Italia kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Hispania, Florentino Perez hakumfanya ajihisi kuwa mchezaji anayethaminiwa Santiago Bernabeu.

Hii picha Ronaldo wakati akiwa Real Madrid

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, amesema kuwa Perez alikuwa akimtazama kwenyemahusiano ya kibiashara zaidi na hicho ndicho anachotambua hivyo kila alichomuambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake.

Image result for Real Madrid president

Rais wa klabu hiyo ya Hispania, Florentino Perez 

”Perez alikuwa akinitazama mimi kwenyemahusiano ya kibiashara zaidi  na hicho ndicho ninachofahamu hivyo kila alichokuwa akiniambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake,” amesema Ronaldo.

Raia huyo wa Ureno ameongeza “Nilisikia ndani ya klabu, hasa kutoka kwa rais mwenyewe kwamba hawakunichukulia mimi sawa na vile walivyofanya wakati nakuja kwenye miaka minne au mitano iliyopita.”

“Rais alikuwa akinitazama, macho yake yakitoa tafsri ambayo haiyendani na kile anachozungumza, kiasi kwamba sikuwa na nafasi tena kwao. Kama unaelewa ninachomaanisha, hicho ndicho kilichonifanya kufikiria kuondoka.”

“Wakati mwingine nilikuwa nikitazama habari, namna wanavyozungumza nilijiuliza kuhusu kuonda. Ni machache tu kati ya hayo lakini ukweli ni kwamba rais asingelinizuia nisiondoke,”

“Kama yote ingekuwa nafanya kwaajili ya pesa basi ningekwenda China mahala ambapo ningeweza kupata fedha nyingi kuliko hata Juve au Real. Sikuja Juve kwasababu ya fedha ningepata sawa tu na Madrid kama siyo zaidi.”

“Tofauti ni kwamba Juve, ni kweli wananihitaji wamekuwa wakiniambia hivyo na nikaamua kuliweka sawa kwasababu wamenithibitishia.’

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amejiunga na klabu hiyo ya Serie A akitokea Madrid kwa dau la euro milioni 100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents