Michezo

Ronaldo akanusha kusimamiwa na kampuni mpya ya michezo ya Lil Wayne

Nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo amekanusha habari zilizosambaa hivi karibuni kuwa amesaini mkataba wa kusimamiwa na kampuni mpya ya usimamizi wa michezo ya rapper Lil Wayne.

Ronaldo

Wiki iliyopita mtandao wa TMZ uliripoti kuwa kampuni mpya ya Weezy itamsimamia Ronaldo shughuli zote za kimichezo kuanzia branding, endorsements, modeling hadi marketing kwa nchini Marekani, akiwa kama mteja wa kwanza.

Ronaldo alitweet kukanusha habari hizo:

“Kumekuwepo na habari kuhusu mabadiliko ya timu yangu ya usimamizi, hayo yote ni uongo, na ninaweza kuwahakikishia timu yangu ni ile ile na itaendelea kuwa ile ile” .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents