Michezo

Ronaldo amgaragaza Messi kwenye Ballon d’Or, Akaribia kukalia kiti chake

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo.

Ronaldo amemshinda mpinzani wake wa karibu anayekipiga kunako klabu ya Barcelona, Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kutwaa kwa mara ya tano.

Kwa ushindi huo sasa Ronaldo na Messi wote wanakuwa sawa kwa kuchukua tuzo hiyo kubwa ya heshima mara tano.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr akishika nafasi ya tatu. Kama kura zinavyoonesha (1. Cristiano Ronaldo -946 pts 2. Lionel Messi -670 pts 3. Neymar -370 pts)

Lionel Messi ndiye mchezaji pekee aliyekuwa mwenye mataji mengi ya tuzo hiyo kabla ya jana Ronaldo kuchukua tuzo hiyo na kumfanya awe naye sawa kitu ambacho endapo Messi atazubaa msimu huu basi ufalme huo wa kumiliki kwa wingi tuzo hiyo huenda akachukua Ronaldo.

Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.

Ballon d’Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents