Michezo

Ronaldo amzima Neymar Bernabeu, Liverpool yatoa dozi ya mwaka Ureno

Mchezo wa Real Madrid na PSG uliochezwa usiku wa Jumatano hii, katika hatua ya 16 bora ya kombe la mabingwa barani Ulaya ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka. Madrid mbao wanaonekna kufanya vibaya kwenye La Liga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika uwanja wao wa Bernabeu.

Mabao ya Mdrid yamefungwa na Cristiano Ronaldo mbaye amefunga mabao mawili katika dakika ya 45 na 83, na Marcelo aliyefunga dakika ya 86. Bao la kufutia machozi la PSG lilifungwa na Rabiot 33.

Wakati huo huo, katika mchezo mwingine Liverpool ambao walikuwa katika uwanja wa ugenini nchini Ureno kuwafuata FC Porto, wameibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Sadio Mane aliyefunga magoli matatu katika dakika ya 25, 53 na 85, Mohamed Salah dakika ya 29,, pamoja na Roberto Firmino aliyefunga bao lake kwenye dakika ya 69.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents