Michezo
Ronaldo aongeza idadi ya warembo aliotoka nao
Christiano Ronaldo ameendelea kuongeza namba ya warembo aliotoka nao.
Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake mshindi wa taji la Miss Hispania 2014, Desire Cordero mchezaji huyo kwa sasa ameibuka na kimwana mpya ambaye ni mwanamitindo anayejulikana kwa jina la Georgina Rodriguez.
Wawili hao walionekana pamoja Jumatano hii huko jijini Paris baada ya mechi ya kombe la Uefa ya Jumanne iliyowakutanisha Sportin Lisbon dhidi ya Real Madrid iliyochezwa nchini Ureno.
Tazama picha za wawili hao wakiwa huko Paris.