DStv Inogilee!

Ronaldo apeleka mageuzi mengine makubwa ligi kuu ya Italia Serie A

Ronaldo apeleka mageuzi mengine makubwa ligi kuu ya Italia Serie A

Akiwa na umri wa miaka 33 akizaliwa february 5 mwaka 1985 mitaa ya Funchal Madeira nchini Ureno,Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro amekuwa na wakati mzuri sana katika karia yake ya soka kwani amefanikiwa kuvunja rekodi mbalimbali licha ya umri wake kuonekana mkubwa.

Ronaldo amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanasoka bora duniani Ballin d’or kwa nyakati tano tofauti 2008,2013,2014,2016 na 2017, huku akifanikiwa kushinda taji la UEFA Champions League kwa nyakati tano pia akizitumikia klabu za Manchester United na kutoka nchini Uingereza msimu 2007/08 huku akishinda kwa nyakati nne katika klabu ya Real Madrid misimu ya 2013/14,2015/16,2017/18 na 2018/19.

Licha ya kuvunja rekondi mbalimbali lakini pia katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid amebakia kuwa mfungaji bora wa muda wote.

Mapema mwaka huu 2018 alifanikiwa kujiunga na klabu ya Juventus kutoka Turin nchini Italia kwa rekodi ya klabu inayofikia euro mil 100,lakini baada ya kujiunga na klabu hiyo Ronaldo amekuwa mchezaji wakwanza katika klabu hiyo kuendelea kulipwa kitita kikubwa zaidi katika klabu yake na pia katika ligi nzima ya Italia alimaarufu Seria A.

Kitendo kinachotafsiriwa na wengi kuwa huenda ndo ikawa neema kwa wachezaji wa ligi hiyo kupanda thamani kwa walionekana kuwa na thamani ndogo sana ukiwalinganisha na wachezaji kutoka katika ligi kubwa tano barani Ulaya,zikiwa ni Ligi kuu nchini Uingereza PL,ligi kuu nchini Uhispania La liga,ligi kuu nchini ufaransa Ligue 1,na ligi kuu nchini Ujerumani Bundasliga.

Na hii ndio orodha ya wachezaji wanaopokea kiasi kikubwa zaidi akimzidi mchezaji anayefuata mara mbili zaidi:-

 

Cristiano Ronaldo ameshacheza michezo minne ya ligi hadi hivi sasa katika klabu yake hiyo mpya ya Juventus  huku akishindwa kufunga hata goli moja akiwa amepiga zaidi ya mashuti 22 golini bila kuzaa matunda.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW