Michezo

Ronaldo arudisha makali yake La Liga, Aipeleka Madrid nafasi ya tatu

Baada ya kuanza msimu mpya wa 2017/18 kwa kusuasua mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana usiku ameonesha makali yake kwa mara ya kwanza tangu uanze msimu huu kwa kupiga hat-trick kwenye mchezo ambao Madrid wameshinda goli 5-2 dhidi ya Real Sociedad.

Hii inakuwa Hat-trick yake ya kwanza kwa msimu huu 2017/18 na inakuwa ya 33 kwenye La Liga na ya 43 kwa Real Madrid kwenye michuano yote aliyoitumikia klabu hiyo.

Magoli mengine ya Real Madrid yamefungwa na Lucas Vazquez na Toni Kroos huku mawili ya Sociedad yakifungwa na Asier Illarramendi na Jon Bautista.

Kwa ushindi huo wa jana Madrid wanakuwa kwenye nafasi ya tatu kwa alama 42 nyuma ya mahasimu wao Atletico Madrid wenye alama 52 na vinara Barcelona wakiwa alama 58.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents