Michezo

Ronaldo ashangazwa na ndoto za mwanae

Waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka, usemi huu unadhihirika pale mtoto wa kwanza wa nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ambaye anatambulika kama Cristiano Jr mara kadhaa akionekana kutamani kuwa kama baba yake.

Hapo jana siku ya Alhamisi staa huyo wa Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo ameposti picha ya mtoto wake katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram ikimuonyesha akiwa kifua wazi huku akitunisha misuli na kuandika kuwa ‘baba nitakuja kuwa kama wewe’.

Katika picha hiyo Cristiano Jr mwenye umri wa miaka saba ametunisha misuli na kuwa na muonekano sawa na ule wa baba yake mwenye umri wa miaka 33.

Wakati wa mahojiano yake na gwiji wa soka, David Ginola mwezi desemba alipotwaa tuzo ya tano ya Ballon d’Or, Ronaldo ambaye ni baba wa watoto wanne amesema kuwa anapo muangalia Cristiano Jr ni kama anajiona mwenyewe.

Ninapo muangalia Cristiano Ronaldo Junior ni kama najiona mwenye na hii si kwasabu mwanangu lahasha bali mara kwa mara huniambia atakuja kushinda mara tano tuzo ya Ballon d’Or na husema atakuja kuwa bora zaidi yangu mimi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents