Michezo

Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa FIFA

Mchezaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya FIFA
Ronaldo, 31, amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.

Ronaldo pia ameshinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi Disemba mwaka jana, kufuatia mafanikio yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016 akiwa na timu ya taifa ya Ureno.

Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri ametajwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, huku Silvia Neid, meneja wa zamani wa Ujerumani, akishinda kwa upande wa wanawake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents