Michezo

Ronaldo astaafu Soka

ronaldo

Gwiji la soka kwa miaka mingi Ronaldo anayetokea Brazil ametangaza kustaafu mpira

 

Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa soka wa FIFA kwa miaka zaidi ya mitatu aliyatangaza hayo alipokuwa mjini Sao Paolo na kuelezea sababu kuu kuwa kusumbuliwa na maradhi mara kwa mara.

Ronaldo aliyewahi kuchezea Real Madrid na Ac Milan za ligi kuu ya Hispania pamoja na timu ya Taifa ya Brazil amesumbuliwa sana na tatizo la goti iliyopelekea kumfanya kuwa na maumivu sana pamoja na maradhi yaliyomfanya kutoweza kuendelea na soka akiwa na umri wa miaka 35.

Habari hizi zimewashtua mashabiki wa soka duniani kote kwani Ronaldo alikuwa mchezaji wa aina yake na atakumbukwa zaidi kwa ustadi aliouonyesha kote katika uchezaji wake.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents