AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Ronaldo atoa ya moyoni aumizwa na ushindi wa United ” Manchester hawakustahili ushindi maana hawakufanya chochote”

Ronaldo atoa ya moyoni aumizwa na ushindi wa United " Manchester hawakustahili ushindi maana hawakufanya chochote"

Mchezaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefunguka na kuongea jinsi alivyoumia baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Manchester katika uwanja wao wa Allienz.

Ronaldo ndio aliyeanza kufunga goli mnamo dakika ya 65 kabla ya goli ya kusawazisha la Juan Mata na goli la kujifunga la Sandro mnamo dakika ya 89,ameongea hayo baada ya mchezo wao wa jana usiku katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya UEFA.

Ronaldo alisema :- “”Ligi ya Mabingwa ni ligi yenye ushindani mkubwa sana, ambapo unaweza kushinda, lakini hauwezi kupumzika, kwani kunaweza kutokea chochote na muda wowote,”

“Tulitawala mchezo kwa dakika 90 zote, tulikuwa na nafasi nyingi za kushinda, ambazo zingetusaidia kuwaua kabisa nafasi za wazi  zilipatika mara tatu au nne, lakini tulifurahi na tukaona tumeshinda mwishowe  tukaadhibiwa.”

“Manchester United haikufanya chochote ambacho kingepelekea kushinda mchezo, Huwezi hata kuongelea ukasema kuwa hii ilikuwa ni bahati, kwa sababu unapaswa kuitengeneza bahati na ukpelekea kupata bahati yako na katika mchezo huu sisi ndo ilitakiwa iwe bahati kwetu, Sasa tunapaswa kuinua vichwa vyetu, kama tulicheza vizuri na bado ni juu ya kundi.”

Mbali na maneno hayo ya Ronaldo kampteni wa Juventus Chiellini alisema :- ” “Tunataka kwenda mbele zaidi na kama tunapaswa kufanya hivyo, lazima tujifunze kutokana na kosa la aina hii”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW