Michezo

Ronaldo atuma zawadi hii kwa Marcus Rashford

Kumbe Cristiano Ronaldo na Marcus Rashford wamekuwa marafiki?

Hutakiwi kushangaa hilo bali huo ndio ukweli wenyewe. Tena mara kadhaa Ronaldo amekuwa akimtumia Rashford baadhi ya zawadi za michezo.

Rashford ambaye anaonekana kuja kuwa mchezaji hatari, kupitia mtando wa Instagram ameonyesha zawadi ya jezi ya Real Madrid aliyopewa na Ronaldo hivi karibuni ambayo pia aliisaini mshambuliaji huyo ambaye amewahi kuichezea Manchester United kwa misimu takribani sita.

“Thanks boss 🙌🏾 @cristiano,” ameandika kwenye mtandao huo.

Lakini pia mapema mwezi huu Ronaldo alimtumia mchezaji huyo zawadi ya viatu vya aina ya Nike Air Max 97 CR7 vyenye rangi nyekundu.

Hata hivyo mara kadhaa Rashford amewahi kusema kuwa Ronaldo ndio mchezaji amekuwa akimtazama kama role model wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents