Michezo

Ronaldo avunja record iliyoshikiliwa kwa miaka 46

By  | 

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo usiku wa jana amefanikiwa kuvunja record iliyowekwa miaka 46 iliyopita na mchezaji , Jimmy Greaves , ya Kuongoza kwa jumla ya Ufungaji wa magoli ya Ulaya na kuisadia klabu yake ya Real Madrid kunusa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania kwa tofauti ya alama tangu 2012.

Ronaldo,mwenye umri wa miaka 31, ameifikisha Madrid kuwa kileleni baada ya kushinda goli lake la 367 katika mabao yake yote ya Ulaya, kwenye ligi kuu tano bora za Ulaya , historia ambayo iliwekwa na Legendari wa Uingereza , mshambuliaji,Greaves mwaka 1971.

Katika mchezo huo ambao Real Madrid ilichomoza na ushindi wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, mchezaji huyo alitupia goli moja kati ya hayo, sasa Madrid inahitaji sare yoyote katika mchezo wake wa mwisho wa ligi wakatapo kutana na klabu ya Malaga jumapili hii , ili kujitangazia Ubingwa wa Ligi.

Mahasimu wao klabu ya Barcelona watalazimika kushinda katika mchezo wao wa mwisho wa nyumbani dhidi ya klabu ya Eibar ili kumtia presha zaidi kocha wa Madrid, Zinedine Zidane, na kama mpaka ligi ikimalizika na klabu hizi kulingana alama basi Barca itakabidhiwa kombe, hii ni kutokana na namna Madrid alivyofungwa zaidi na Barca timu hizi zilipokutana, hivyo Barca itakuwa inachukua ubingwa huu mara ya 3 mfululizo.

Katika Mchezo wa hapo Jana Real Madrid imeonekana kuzidiwa licha ya Ushindi walioupata.

Maneno ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane.

‘Sijiskii kama vile tumeshakuwa mabingwa hapana bado

“Tumesalia mchezo mmoja lakini siku ya leo ilikuwa muhimu sana . Tunafahamu ni ni tunahitaji kufanya . Tunahitaji kujiandaa vyema na kujiweka sawa kuanzia leo”.

Goli la 367, la Cristian Ronaldo katika mchezo wao na Celta Vigo uliomalizika kwa matokeo ya 4 kwa 1

“Namna ya dakika 45 za kipindi cha kwanza zilivyoisha zinatufanya tusijiskie vizuri, tulikuwa wazuri zaidi katika kipindi cha pili lakini tulicheza kidogo”.

“Sihitaji kujiskia kama tayari sisi ni Mabingwa, bado tunahitaji alama zaidi na hicho ndio kitu tunachotaka kufanya”.

BY HAMZA FUMO

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments