Ronaldo aweka rekodi mpya duniani, afikisha wafuasi milioni 250 Instagram

Mchezaji kandanda wa Ureno na klabu ya soka ya Juventas Christiano Ronaldo anazidi kuandikisha historia na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mtu wa kwanza duniani kufikisha wafuasi milioni miambili na hamsini katika mtandao wa instagram. Christiano ambaye hivi majuzi alijinyakulia ubingwa wa kuwa mchezaji bora wa karne hii, anazidi kujizolea umaarufu kila kona ulimwenguni.

Ronaldo alishawahi kuichezea timu ya Manchester united ya Uingereza, Real Madrid ya Uhispania na sasa yupo nchini Italia akichapa kabumbu ya kulipwa kupitia klabu yake ya Juventus ambayo inafanya vizuri sana na imekua ikitegemea sana huduma za nyota huyu wa kutoka nchini Ureno.

Mara nyingi Ronaldo amekua akishindanishwa na mchezaji wa Argentina na klabu ya Barcelona- Lioness Mess ambae pia anang’ara sana haswa kwenye ulingo huu wa mchezo wa kabumbu.

Imeandikwa na @changez_ndzai – Kenya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW