Michezo

Ronaldo chupu chupu kujiunga na Arsenal, mwenyewe afunguka ”Mnisamehe The Gunners, hususan Arsene Wenger ”

Mchezaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amesema kuwa ilikuwa bado kidogo tu angejiunga na washika mitutu wa Londo timu ya Arsenal kabla ya kutua Manchester United mnamo mwaka 2003 huku akimpongeza aliyekuwa kocha wa timu hiyo kwa wakati huo Arsene Wenger.

Cristiano Ronaldo has admitted he had come 'one step away' from joining Arsenal in 2003

Mshambuliaji huyo wa taifa wa Ureno amefunguka kuwa, alikuwa kwenye hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa kutua ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa jiji la London wakati huo akiwa na umri wa miaka 18, lakini badala yake akaamua kujiunga na Old Trafford akitokea Sporting Lisbon.

Ronaldo ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na mwandishi wa habari wa ITV, Piers Morgan lakini pia kutumia nafasi hiyo kuwaomba radhi mashabiki wa Arsenal kwa kitendo hicho cha kutokujiunga na klabu yao.

 The forward opted for Man Utd in 2003

Kcha wa Manchester United kwa wakati huo, Sir Alex Ferguson alihakikisha kipaji cha kijana huyo kinatua Old Trafford.  Akiwa Manchester United, Ronaldo amewezesha timu hiyo kutwaa mataji matatu ya Premier League titles na moja Champions League.

Alipoulizwa kama ni kweli alikuwa anakaribia kusaini Arsenal, Ronaldo alikiri kuwa ni kweli tena ilikuwa karibu mno kujiunga nao. Morgan alimtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, kuwaomba radhi mashabiki wa Arsenal kwa kuwavunja moyo wakati huo alipokuwa akitarajiwa kujiunga nao na badala yake akajiunga na United.

“Ilikuwa nakaribia kabisa kujiunga na Arsenal, tena karibu sana. Naomba radhi kwa mashabiki wa Arsenal, sawa.” Amesema Ronaldo.

“Mnisamehe kwa kutojiunga na Arsenal, hivi ndivyo inavyotokea zilikuwa ni ndoto za miaka 16 nyuma, lakini bado hawajachelewa.”

Ronaldo aliongeza “Isingelitokea lakini na heshimu Arsenal kwa kile walichonifanyia kwangu, husuan Arsene Wenger lakini kama unavyofahamu kwenye soka huwezi jua kitakachotokea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents