Michezo

Ronaldo hawezi kuja Manchester United – Mourinho

By  | 

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema kamwe hawezi kukaa na kufikiria ujio wa mchezaji Cristiano Ronaldo  ndani ya timu yake.

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho

Mourinho ameyasema hayo wakati akiwa na United katika ziara yake huko nchini Marekani. “Siwezi kupoteza muda wangu kumfikiria mchezaji ambaye uhamisho wake hauwezekani (mission impossible),” Mourinho aliyasema hayo mara baada ya baada ya mchezo wake wa kirafiki.”

Manchester United imepata ushindi wake wa kwanza katika ziara yake huko Marekani wikiendi hii baada ya kuifunga La Galaxy kwa magoli 5-2. Meneja huyo wa United anaamini kikosi chake kwa sasa kipo imara baada ya kuongeza wachezaji, Victor Lindelof kutoka Benifica na Romelu Lukaku kutoka Everton.

By Hamza fumo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments