Ronaldo kumkaribisha Pep Guardiola Juventus

Imeripotiwa kuwa miamba ya soka ya Italia, Juventus inajipanga kumng’oa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola

Inadaiwa vigogo hao wa Serie A, pesa kwa sio tatizo na wapo tayari kutoa kiasi chochote ambacho Mhispania huyo, Guardiola atakitaka ili mradi tu kukamilisha mipango yao.

Kulingana na ‘The Sun’ Juve inampango wa kuachana na Maurizio na kumkaribisha, Guardiola kama kocha Mkuu wa klabu hiyo.

Pep Guardiola is being linked with an audacious Juventus move to replace Maurizio Sarri

Kumbuka tu Juventus kwa sasa inamchezaji bora kabisa duniani Ronaldo ambaye ni hasimu mkubwa wa nyota wa Barcelona, Messi hivyo kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kama dili hilo litatimia Guardiola atakuwa amewafundisha wababe hao wawili katika ramani ya soka kwa nyakati tofauti.

Rais wa Juve, Andrea Agnelli tayari amesema kuwa Guardiola ndiye mtu pekee aliyekosekana kwenye timu hiyo ambaye ataweza kuleta ubora upande wao.

Tayari Inter, inaongoza ligi ikiwa chini ya Antonio Conte, na hivyo kumfanya kocha, Sarri kukalia kuti kavu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW