DStv Inogilee!

Ronaldo kurejea uwanjani kuikabili Udinese, kocha wa Juventus amwagia sifa 

Mshambuliaji hatari duniani anaekipiga ndani ya klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo anatarajiwa kurejea uwanjani hapo kesho kuikabili timu ya Udinese.

Nyota huyo hatari kunako mchezo wa soka anakabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanadada, Kathryn Mayorga raia wa Marekani ambaye amesema kuwa kitendo hicho amefanyiwa mwaka 2009 huko Las Vegas.

Licha ya timu ya taifa ya Ureno kutangaza hapo jana kuwa haitamjumuisha Ronaldo ndani ya kikosi hicho, mchana huu meneja wa klabu ya Juve, Massimiliano Allegri  amethibitisha kuwepo kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 hapo kesho.

“Namfahamu Cristiano kwa miezi mitatu sasa na kwazaidi ya miaka 15 katika fani yake amekuwa akionyesha taaluma bora ndani na nje ya uwanja. Yupo tayari kwa kurejea hapo kesho,” amesema Allegri.

Siku ya Jumanne Ronaldo alikuwa nje ya uwanja akishuhudia timu yake ya Juve ikiibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 0 dhidi ya Young Boys michuano ya Champions League baada ya kupewa adhabu ya kutocheza mechi moja kutokana na kumtendea mazambi mchezaji wa Valencia.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW