Michezo

Ronaldo: Nitabaki Real Madrid hadi mkataba wangu utakapo isha

Mchezaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema hawezi kuondoka klabuni hapo kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka 2018.

30FA8CCC00000578-0-image-a-89_1454947981802

Amekua akihusishwa na kurudi kujiunga na timu yake ya zamani ya Manchester United, ambayo ilimuuza mwaka 2008 au Paris St-Germain, ya Ufaransa.

“Nataka kubakia hapa kwa miaka miwili zaidi, miaka miwili ninayozungumzia itanichukua mpaka mwisho wa maktaba wangu, “alinukuliwa mchezaji huyo.

Ronaldo alizungumza hayo wakati ya ghafla ya uchukuaji tuzo ya Pichichi, ambapo alishinda tuzo hiyo baada ya kuwa mfungaji bora msimu uliopita kwa kufunga mabao 48.

“Hii ni ligi bora duniani, japo kuwa pia nimecheza ligi ya England, ni ligi ya ushindani na inawachezaji wazuri.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents