Michezo

Ronaldo wa Mbeya City atunzwa kiroba cha mchele kwa kupeleka majonzi Jangwani

Mara baada ya mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City, Iddy Seleman ‘Ronaldo’ kuisawazishia timu yake dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC mashabiki wa timu hiyo wamemtunukia kiroba cha mchele mchezaji huyo.

Ronaldo amesema kuwa mashabiki wa Mbeya City wamemfanyia ‘suprize’ kwa kumpatia zawadi ya Mchele, Ndizi kama shukrani ya kupeleka msiba Jangwani ambao wanahaha kuhakikisha wanaifukuzia Simba SC kwenye mbio za msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nilikuwa nasikia kwa wachezaji wenzangu kwa namna mashabiki wa Mbeya walivyo wakarimu kama ukiwafurahisha.

Nilichokiona baada ya kurudi kambini kilinishangaza kwelikweli, mashabiki wameleta mchele, ndizi.

Ronaldo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram ameongeza kwa kumshuku Mungu na kumuomba amjaalie zaidi.

Asant mungu nakuomba nijalie zaid ya ivi ulivo nipa asante muweza wayote Mora tabalaka

Mchezaji wa Mbeya City, Iddy Seleman akiwa ameruka juu kuufuata mpira

Iddy Seleman ‘Ronaldo’  ni zao la Ndondo Cup kupitia timu ya Misosi FC yenye maskani yake mitaa ya  Tandale na mara kadhaa amewahi kuwa mfungaji bora na mchezaji bora wa Ndondo Cup.

Tayari baadhi ya klabu zinazoshiriki ligi kuu zimeanza kumtolea macho, Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara moja ya maelezo yake amesema kuwa huwenda wakamsajili  kwa ajili ya klabu bingwa Africa mwakani endapo atapunguza usela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents