Michezo

Ronaldo, Zidane wang’ara tuzo za FIFA (Picha)

Mshambuliajia wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amelitetea tena taji lake la mwanasoka bora wa Fifa kwa mwaka wa pili mfululizo.

Ronaldo amemshinda Lionel Messi ria wa Argentina anayekipiga Barcelona aliyeshika nafasi ya pili.

Nafasi ya tatu imekwenda kwa mwanasoka ghali zaidi duniani, Neymar kutoka Brazil anayekipiga PSG ya Ufaransa.

Ronaldo ambaye ameiwezesha klabu yake ya Real Madrid kutwaa taji la ligi ya Hispania La Liga na lile la klabu bingwa barani Ulaya amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 44 katika michezo 48 ndani ya klabu na nchi yake.

Alifunga mabao mawili katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus huko Cardiff  June 3 na kuiwezesha Real Madrid ya kuweka rekodi ya kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili mfululizo likiwa ni kombe lao la 12.

Baada ya tuzo hiyo Ronaldo amesema “Naziitaji saba. Tano nilizopata mpaka sasa ni vizuri lakini saba ni namba yangu ya bahati kwahiyo kuzipata saba itakuwa vizuri zaidi.”Amesema mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid.

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametwaatuzo ya kocha bora wa mwaka. Zidane amenyakua tuzo hiyo kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kikosi chake baada ya kushinda ubingwa wa La Liga na Klabu bingwa barani Ulaya mara ya pili mfululizo.

Katika tuzo hizo za FIFA zilizo tolewa hapo jana usiku Jijini London naye mlinda lango mkongwe wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi “Gigi” Buffon ametangazwa kuwa kipa bora wa FIFA na mara baada ya kupokea tuzo hiyo kipa huyo amesema “Nazungumza kwa Kiingereza,  nikipindi kigumu sana hiki,” amesema Buffon mwenye umri wa miaka 39.

Mlinda lango mkongwe wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi “Gigi” Buffon

Buffon ameongeza “Ni heshima kubwa sana kupata tuzo hii katika umri huu hakika najivunia msimu uliyopita ulikuwa na changamoto kwa Juventus na hata kwangu na lishindwa hata kutwaa taji la Ulaya. Ningelipenda hata tumalize na Ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi nikiwa na Italia.”

Usiku huo wa Jumatatu ulikwenda vizuri pia kwa mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud kunyakuwa tuzo ya Puskas ambayo hukabidhiwa kwa mchezaji aliyefunga bao bora la mwaka.

Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amekabidhiwa tuzo hiyo ya Puskas baada ya kushinda bao safi maarufu kama ‘scorpion-kick’ dhidi ya Crystal Palace mwezi Januari mwaka huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents