Michezo

Rooney aifukuzia rekodi ya Sir Bobby Charlton kwenye FA

Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ataanza dhidi ya Reading mechi za raundi ya tatu Kombe la FA.

Muingereza huyo alikosa mechi tatu za Ligi Kuu kipindi cha sikuu ambazo United ilishinda zote baada ya kupata majeraha ya misuli ya paja kwenye mazoezi siku ya Krismasi.

Meneja wa United Jose Mourinho amebainisha kuwa wachezaji hao watacheza katika mechi hiyo itakayopigwa katika uwanja wa Old Trafford, akiongeza kuwa ana kikosi kipana cha kufanya uchaguzi.

Rooney atakuwa anaifukuzia rekodi ya muda wote ya kufunga magoli na huenda akapata fursa ya kuifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton mbele ya legendari huyo wa Mashetani Wekundu anayetarajiwa kuushuhudia mchezo huo.

Luke Shaw pia atakuwepo baada ya wiki kadhaa za kupambana kurejea kwenye afya yake na Daley Blind pia atakuwepo kwa mara nyingine baada ya kuikosa West Ham na kipa wa ziada Sergio Romero ataanza katika mchezo wa leo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents