Michezo

Rooney amkabidhi mikoba Harry Kane, asema anaamini mchezaji huyo atavunja rekodi yake

Rooney mwenye umri wa miaka 33, alirudi uwanjani kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa ya 120 na ya mwisho akiwa na timu ya taifa ya soka ya Uingereza.

Katika mechi hiyo Uingereza walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Marekani huko Wembley siku ya Alhamisi lakini mchezaji huyo hakubaatika kufunga goli. Rooney alisema: “Kama ningefunga huenda goli hilo lingeleta mjadala mwingine kuhusu kama goli hilo lingehesabiwa au la, hivyo labda ilikuwa jambo jema!”

Mshambuliaji huyo wa timu ya DC United ndiye mchezaji aliyefungia mabao 53 timu ya Uingereza katika michuano mbalimbali ya kimataifa.

Rooney amesema kwamba matamanio yake kwa sasa ni kutamani kuwasilisha tuzo kwa Harry Kane.

Mchezaji huyo wa zamani wa Everton na Manchester United  alianza kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza akiwa na umri wa miaka 17 dhidi ya Australia mwaka 2003, na kustaafu mpira wa miguu wa kimataifa mwaka 2017.

Wayne Rooney, England.

 

Chama la Soka FA  liliona mechi ya Uingereza dhidi ya Marekani iliyochezeka jana  Alhamisi kama fursa ya kutoa heshima yao kwa mchezaji huyo kwa kazi yake ya kuvunja rekodi ya kimataifa.

Kane na mwenyekiti wa FA Greg Clarke waliwasilisha tuzo kwa Rooney kabla ya mchezo huo.

Rooney alisema: “Nilimwomba Harry anikabidhi tuzo kwa sababu ninaamini yeye ndiye mchezaji atayevunja rekodi yangu ya kimataifa.”

 

Na Raheem Rajuu

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents