Michezo

Rooney ashindwa kuisaidia Everton Goodison Park

Klabu ya Everton inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa hapo jana ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Goodison Park ilikubali kipigo kibaya cha mabao 5-2 dhidi ya Arsenal mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Waliyoihangamiza ngome ya Everton usiku wa jana walikuwa ni wachezaji,Mesut Ozil, Nacho Monreal , Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey wakiifungia Arsenal wakati Wayne Rooney akiifungia The Toffee bao lake la kwanza wakati lapili likifungwa na Oumar Niasse.

Kwa matokeo hayo Everton mpaka sasa inakuwa imepoteza idadi ya michezo mitano wakati Arsena ikipaa kileleni hadi nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents