Burudani

Rosa Ree aeleza sababu ya AY na Diamond kumkubali

Only Female Rapper kutoka label ya The Industry, Rose Ree ameeleza sababu ya wasanii wakubwa kuubali muziki wake. Katika nyakati tofauti wasanii kama AY na Diamond walionyesha kuvutiwa na uwezo wa Rapper huyo.

Rosa Ree amesema utofauti aliokuja nao katika game umependwa na wengi kwa sababu hakuufikiria muziki wake katika level ya Bongo bali alitaka muziki wa Bongo ufike mbali.

“Kupitia Rosa Ree muziki wa hip hop uweze kutusua kwenye anga za juu zaidi kwa sababu sijawahi kusikia tumejulikana huko nje Tanzania tunafanya hip hop, nataka tufike kwenye Grammy na Oscar,” Rosa Ree ameiambia Twenzetu ya Times Fm na kuongeza.

“Kwa sababu hiyo all in all nitaendelea kuwa real na ninashukuru watu wanaendelea kupokea kwa sababu sikutarajia watu wakubwa wanaweza kuukubali muziki wangu, kwanza hata Nahreel alivyonicheki wewe upo vizuri nilijisikia vizuri,” amesisitiza.

Rose Ree alitambulika katika Bongo Flava kupitia ngoma yake ya One Time ambayo remix yake amemshirikisha Khaligraph Jones kutoka Kenya, kisha akatoa Up In The Air na sasa anatamba na ngoma mpya ‘Mchaga Mchaga’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents