Bongo Movie

Rose Ndauka asilimu dini kisa Love la Mbongo fleva

rose_ndauka

Katika kukuwa kwa tasnia za muziki wa Bongo Fleva na filamu Tanzania kumepelekea hata wasanii na wao kuingiliana katika kazi na hata  kuzichanganya pamoja. Wapo waigizaji waliogeukia na muziki kama Shilole, pia wapo wanamuziki wamegeukia uigizaji


kama H.Baba. Hawa wanaweza kuwa  mifano mizuri kati ya wasanii wengi ambao wanachanganya, hasa katika kusaka mshiko ili kula sahani moja na hali harisi ya maisha.

Bado hawakuishia katika kuingiliana katika kazi za  kisanii ila wameamua kufika mbali zaidi katika maisha, huenda wapo wanafanya kweli na wapo wamegeuza kama  fasheni yaani msanii wa filamu kuwa na uhusiano na msanii wa muziki.

Hivi juzi mwanamuziki Rose Ndauka, ametangawa wazi kwamba anauhusiano wa kweli na unaojulikana hadi kwa wazizi na mwanamuziki  Maliki Bandawe. Hapa tunasema ameungana na mwigizaji mwenzake  wema katika kutangaza wazi kwamba amezama in Love na waimbaji wa Bongo Fleva Diamond.

Wema yeye alikubali kuvishwa pete, huku tukisikia stori za wengine kama  mwigizaji Jack wa Chuzi na mbongo fleva Timburo  na hata marachache tulisikia ya mbongo fleva  Barnaba na na mwigizaji Shilole.

Huu ni wakati wa Rose Ndauka, ambaye kwa sasa ameshabadili jina na kuitwa Aisha, Kama ilivyokuwa  kwa Witnes kubadili dini kwaajili ya Monkeyz.

Ila Rose Ndauka amesema yeye amebadili dini kwaajili  mama yake kuwa muislam, lakini pia kwa upande mwingine ni msukumo wa kijana toka Tanga… yaani Tanga yalikozaliwa mapenzi Maliki.

Hivi sasa Rose amesema anapenda kuitwa Aisha ingawa kwenye tasnia ya filamu atajulikana kama Rose Ndauka. Na ukitaka kumjua bwana wake hebu muangalia katika wimbo wa Bongo. Com ya TNG Squad  kikundi kilichokuja kwa kasi kikalewa na umaarufu kikavunjika(Jamaa aliyevaa kofia mwenye sauti nzito upande wa Chorus).

Hongera Rose Ndauka kwakuwa umesikika ukisema kwamba hutobadilika tabia,  na hutishiki na kauli ya ndoa za mastaa hazidumu.

By Moe One’s

 {hwdvs-player}id=1686|width=560|height=340{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents