Michezo

Rosicky kukaa nnje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na jeraha

Kiungo wa kati wa kilabu ya Arsenal Tomas Rosicky atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na jeraha.

140224142216_tomas_rosicky_512x288_allsport_nocredit

Mchezaji huyo mwenye umri wa 35 ambaye kandarasi yake inakamilika katika msimu wa joto,alipata jeraha jingine la paja wakati wa mechi dhidi ya Burnley siku ya jumamosi baada ya kipindi cha miezi saba akiuguza jereha.

Mchezaji huyo wa taifa la Czech alijiunga na Arsenal mnamo mwezi Mei mwaka 2006.

Alipoulizwa iwapo Rosicky ameichezea Arsenal mechi yake ya mwisho,Wenger alijibu:Natumai hapana ,lakini jeraha hilo ni baya sana.Rosicky ambaye aliichezea Arsenal mara 246 alisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu uliopita.

Wenger amethibitisha kwamba mshambuliaji Danny Welbeck atarudi kuwachezea wachezaji wa Arsenal wasiozidi umri wa miaka 21 siku ya ijumaa.

Mchezaji huyo wa Uingereza,mwenye umri wa miaka 25,ameukuwa nje kwa jereha tangu mwezi Aprili 2015 baada ya kupata jeraha hilo katika mechi iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents