Royal Cellege watembelea kiwandani Mwananchi Communication
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari ya utangazaji cha Royal College of Tanzania, baada ya kutoka kwenye sehemu nzima ya uandaaji wa habari kwenye magazeti Mwananchi, mwana sport la Tanzania na Kenya na Citizen sasa waliwapelekwa wanafunzi hao wa chuo hadi kiwandani.
Huko walionyeshwa jinsi gazeti linavyochapwa na kutoka hadi wasomaji linavyowafikia likiwa tayari.
Kwanza ndugu Edo, aliwapokea na kuelekeza kwamba baada ya gazeti kutoka kwenye matayarisho yote basi huja kiwandani na kufikia kwenye chumba kingine chenye komputa kupitia mtandao.
Anasema komputa hiyo itachoma kurasa moja yaani ile ndefu ambayo inakuchunjwa kati kati, katika hii aluminiam ambayo wanaiita Plat zikiwa nne. anasema kwa kawaida kiwanda kinakuwa na rangi nne, bluu, njano, nyeusi na kijani na zingine zote ni mchanganyiko wa rangi hizo. hivyo kila plat itakuwa ikiwakilisha rangi moja….
Baada ya hapo wanachuo wakasogea kwenye mashine yenyewe kabisa, na haya unayoyaona hapa ndiyo makaratasi ambayo baadaye huwa magazeti yenyewe..
Hapa tayari, makaratasi meupe yakianza kuingia mtamboni kwaajili ya kuchapwa, ili kuonyesha picha na maandishi.
Kisha wakatembelea sehemu ya kuweka rangi,
Safari ikafika hadi sehemu ya kuchapa maandishi kwa kuweka rangi nyeusi…
Taratibu wakashuka ngazi baada ya kuonyeshwa mawili matatu..
Na wengine wakaamua kupiga picha huko huko juu, huyu wa kushoto ni mwanachuo Mohamedi Mussa Gomesa na raisi wa chuo Edwin
N ahapa akionyesha ni jinsi gazeti linavyoonekana baada ya kuchapwa na kutiwa rangi
Huu ni mtambo maalum ambapo magazeti yote yakiwa yanatembea kwenye mzunguko wake, wenyewe watakuwa wakiyaona kwenye scrini hapo juu kidogo..
Mwisho magazeti yote utemwa huku kupitia mkanda maalum wa kuyatembeza, na huku hukutana na wapangaji ambao wanayapeleka sokoni kwaajili ya biashara zaidi…