Tupo Nawe

Rubani wa jeshi aangukia kwenye nyaya za umeme baada ya kujirusha kutoka angani

Ndege ya kijeshi iliyoanguka huko kaskazini magharibi mwa Ufaransa, ilisababisha rubani mmoja kuruka na kuangukia katika nyaya za umeme.

Image result for military airplane france Brittany Pluvigner

Rubani wote waliruka katika ndege hiyo katika eneo la Brittany. Vyombo vya habari  nchini Ufaransa vimeripoti kuwa tukio hilo lilitokea karibu na Pluvigner.

Rubani huyo aliyeangukia umeme, sasa anaendelea vizuri na amenusurika na kupigwa shoti za umeme .

Rubani wote wawili wako salama na wanaendelea vizuri. Nyaya za umeme ambazo mtu huyo aliziangukia zilikuwa na nguvu ya volts 250,000, vyombo vya habari nchini humo vimetaarifu.

Map of Brittany

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeonyesha picha ya namna parachuti ilivyokuwa inashuka karibu na nyaya za umeme.

Picha nyingine zimeonyesha moshi ukiwa unatokea karibu na eneo ndege hiyo ilipopata itilafu katika paa la nyumba moja.

Picha nyingine , inaonyesha ndege ikiwa inawaka moto. Ndege hiyo ya jeshi inaripotiwa kuwa haikuwa imebeba silaha.

Image may contain: tree, outdoor and nature

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW