Burudani

Ruby adaiwa kunasa ujauzito

By  | 

Ikiwa amekaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma wala video, kuna taarifa zimeibuka kuwa msanii wa muziki Ruby ni mama kijacho.


Hii ni moja ya picha ya msanii huyo aliyoianika mtandaoni

Kwa mujibu wa vyanzo vya yetu vimeeleza kuwa mkali kutoka Bongo amekuwa kimya kutokana na kuwa ni mama kijacho,na hata ukipita katika baadhi ya picha zake katika mitandao unaona amekuwa akiongelea kuhusu suala la kuwa mama na kuweka picha za ujauzito.


Husna Abdul, Tunda na Linah Sanga

Endapo kama kweli ni mama kijacho msanii huyo atakuwa ameingia kwenye orodha ya watu maarufu wenye vibendi, kama vile Tunda, Linah Sanga, Husna Abduli na wengineo.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments