Burudani

Ruby ataja vitu vinavyomtofautisha na wasanii wengine wa kike

Ruby amefahamika na kujipatia sifa kede kede kwa wimbo wake Na Yule na pia kwa uwezo wake wa kipekee wa kuimba live.

11374471_1615360765378182_1634968481_n

Tumezungumza na msanii huyo kutaka kujua anajitofautisha vipi na wasanii wengine wa kike nchini.

“Tofauti yangu ya kwanza I do love music first, muziki ambao mimi nimeukuta huku sio live kwanza, mwingi ni playback,” amesema Ruby.

“Mimi napenda kufanya live music na nimekulia katika live music sijakulia katika muziki wa kutumia CD. Halafu I am very unique pia kwasababu mimi ni Ruby hakuna Ruby mwingine kwenye hii industry,” aliongeza.

Ruby amesema wimbo wake mpya unaitwa Sijutii na utatoka hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents