Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Ruto afuata nyayo za Rais Uhuru: Akimbia mdahalo

Makamu wa Rais nchini Kenya, William Ruto ameweka wazi kuwa hatashiriki mdahalo uliopangwa kufanyika leo kwa kusema kuwa hakupata taarifa mapema.

Ruto na Uhuru Kenyatta wakiwa kwenye kampeni huko Lamu leo mchana

Mdahalo wa wagombea wenza kati ya Ruto kutoka Jubilee na Kalonzo Musyoka kutoka muungano wa upinzani (NASA) ulipangwa kufanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.

“Nimeshangazwa hakuna mtu aliyewasiliana nami kuhusu mdahalo huo. Utaratibu unataka kwamba siku, muda na kanuni zitakazotumika zilipaswa kuwekwa wazi mapema kwa wahusika,” ameandika Ruto kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Makamu huyo wa Rais ambaye anawania kurudi madarakani, amesema halikuwa jambo la haki kwa yeye kusikia kuhusu mdahalo huo kupitia mitandao ya kijamii badala ya kuambiwa rasmi na waandaaji.

Ni sawa! Basi sawa, nawatakia kila la heri wale walioshirikishwa. Nadhani kutakuwa na sababu ya kutotendewa haki wote,” amesema Ruto leo mchana kwenye mikutano ya kampeni inayoendelea kwenye miji ya Lamu na Tana River .

Kwa upande wao, waandaaji walisema waliandika barua yenye maelezo kuhusu mdahalo huo na kupeleka ofisi ya Makamu wa Rais.

Tulimwandikia. Ofisi yake ilipokea barua na ilitiwa saini,” alisema Wachira Waruru Mkurugenzi wa kampuni ya Debates Media.

Mapema, mkurugenzi wa mawasiliano ya kidigitali wa Ikulu, Dennis Itumbi, alisema Makamu wa Rais hatahudhuria na badala yake ataendelea na Kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 8.

Mpaka sasa bado haijafahamika kuwa Mgombea mweza, Kalonzo atahudhuria au laa!!

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW