Burudani

RWANDA: Diamond ashangazwa na kipaji cha mtoto mwenye ulemavu wa macho (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameshangazwa na uwezo wa mtoto mwenye ulemavu wa macho huko nchini Rwanda baada ya mtoto huyo kuimba nyimbo zake mbili ile hali hata hajui lugha ya kiswahili.

Diamond akiwa na watoto wenye ulemavu wa macho mapema leo jijini Kigali, Rwanda

Diamond Platnumz ambaye yupo nchini Rwanda kwa ziara yake binafsi ameshangazwa na mtoto huyo kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa macho (Vipofu) cha Jordan Foundation huko Gatsata, Jijini Kigali.

Tazama mtoto huyo alivyomkosha Diamond Platnumz kwa kuimba nyimbo mbili za Je, Utanipenda na Marry You. (Video by Igihe Tv)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents