BurudaniVideos

Sa Raha afunguka maisha yake

Sa_Raha
Mwanamuziki mwenye uraia wa Sweden ambaye anafanya kazi zake za muziki hapa nchini, Sara Ludsrom ‘Sa Raha’,  amesema amevutiwa sana na lugha ya kiswahili na ndiyo maana imemvutia sana kufanya kazi hapa nchini. amesema lugha hiyo imemvutia sana hasa kwenye kuitumia kwenye muziki, kwa kuwani lugha ya Kiswahili imekuwa ikikubali kila mtindo wa muziki ukiimba.


Amesema kwa sasa yeye yupo hapa nchini na mumewe Fundi Samweli, ambaye ni Msweden mwenzake, ambaye wamaeamua kufungungua studio kwa kuhakikisha wanafanya kazi vizuri ya muziki wa Bongo Fleva.

Amesema mumewe amesomea muziki katika chuo cha Sweden, na pia muimba wa muziki wa Rock, na yeye pia alikuwa mwanamuziki wa Ragge na Pop. anasema kwa sasa Sweden na nchini nyingin duniani wamekuwa wakihitaji radha tofauti ya muzki, na yeye alivutiwa sana na radaha ya Bongo fleva kutokana na lugha ya kiswahili.

anasema kwa sasa ameshakamilisha wimbo wake mpya wa Tanesco, ambao unaelezea maisha ya mapenzi yanavyoweza kukwamishwa na masuala ya umeme.  amesema hadi sasa tayari ameshashiriki katika nyimbo mbali mbali kama vile My Dear wa Akili the Brain,  Fei wa Fid Q, Mchumba mwingine wa Jah Man na Nipe Kidogo wa Magese.

amesema pia kwa sasa mumewe na yeye wamefungua studio kwaajili ya kusaidia wasanii wa Kibaha na Picha ya Ndege. anasema tayari ameshakamilisha alba,mu ya mwanamuziki mmoja ambaye ni Abb single, ambayo inaitwa Wanaulizana, ambayo itakuwa na nyimbo kati ya 10 na 12.

Anasema yeye pia ni mpigaa gitaa na ngoma.
Sarah_face

 

{hwdvs-player}id=1659|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1660|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1661|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1662|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1663|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1664|width=560|height=340{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1665|width=560|height=340{/hwdvs-player}

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents