Siasa

Sababu 3 Bush kuja Tanzania hizi hapa

Mahusiano imara kati ya Tanzania na Marekani ni miongoni mwa sababu kubwa tatu zilizosababisha Rais George Bush wa Marekani kuja nchini mwezi ujao.

Na Flora Wingia

 
Mahusiano imara kati ya Tanzania na Marekani ni miongoni mwa sababu kubwa tatu zilizosababisha Rais George Bush wa Marekani kuja nchini mwezi ujao.

 

Hayo yalisemwa jana na Balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green, alipozungumza na wahariri toka vyombo mbalimbali vya habari kwenye ofisi za ubalozi huo, jijini Dar es Salaam.

 

Rais huyo wa taifa lenye nguvu zaidi duniani, pia atazitembelea Rwanda, Benin, Ghana na Liberia katika ziara ya siku sita itakayoanza Februari 15 hadi 21, mwaka huu.

 

Balozi Green alitaja sababu nyingine ya ujio wa Rais Bush kuja nchini kuwa ni kusisitiza mapambano dhidi ya magonjwa ya Ukimwi na Malaria ambayo yanasumbua jamii ya Watanzania.

 

Nyingine ni imani yake kubwa na mustakabali imara wa Tanzania ambapo ina amani, utawala imara na utulivu na kwamba anaamini ziara yake itakuwa kivutio na fursa kwa wawekezaji wa Marekani kuijua Tanzania.

 

Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa upinzani juu ya ujio wa Rais Bush, alisema ni mapema mno kuzungumzia hilo ila alisema haji kama mtu binafsi, bali kama kiongozi wa Marekani ambaye anataka kujenga uhusiano mzuri na Tanzania.

 

Kuhusu iwapo ziara hiyo ni ya kutafuta uwezekano wa Tanzania kuwa makao makuu ya Jeshi la Marekani barani Afrika maarufu kama Africom, Bw. Green alisema “huo ni upuuzi mtupu“ na kwamba hajawahi kusikia mtu akizungumzia jambo hilo.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents