Michezo

Sababu mbili kubwa za kocha wa Chelsea Maurizio Sarri kukataa kupanda basi moja na wachezaji wake baada ya kipigo cha goli 4


Klabu ya Chelsea Jumatano usiku ilikubali kipigo kizito cha goli nne bila majibu kutoka kwa klabu ya Bournemouth. Kipigo hicho ni kikubwa zaidi kwa Chelsea kwa kipindi cha miaka 23 kwenye Ligi ya Premia. Kipigo kikubwa cha ‘mbwa koko’ ambacho Chelsea ilipokea ilikuwa Septemba 1996 walipofungwa 5-1 dhidi ya Liverpool.

Baada ya kipigo hicho kocha wa Chelsea Muitaliano Maurizio Sari alikataa kupanda basi moja na wachezaji na inaelezwa hizi ndio Sababu mbili kubwa za nini Maurizio Sarri alikataa kusafiri basi moja na wachezaji na badala yake aliamua kusafiri peke yake baada ya Blues kushindwa na Bournemouth
Ripoti mpya imesema kuwa baada ya Maurizio Sarri kuwa na majadiliano ya zaidi ya dakika 40 na wachezaji wa Blues, kocha alirudi peke yake Stamford Bridge badala ya kususia basi la timu.

Hatua hii mpya kutoka Maurizio Sarri inaweza kusababisha majibu mawili tofauti, ambayo ni

Jambo la kwanza ni kwamba Maurizio Sarri anaweza kujizuia kutoka kwa timu nzima kwa kuchukua gari badala ya basi ili kumwezesha kufikiri bila ya kelele kutoka kwa wachezaji baada ya kushindwa kupata matokeo dhidi ya Bournemouth.

Sababu nyingine, ambayo hata hivyo inaonekana kuwa mbaya zaidi ni kwamba kunaweza kweli kuwa na ugomvi katika timu tayari kati yake na wachezaji au na viongozi.

Kwa mujibu wa ripoti, wenzake wanaamini kwamba mtindo wa soka wa Sarri unaweza kushindwa na wachezaji na sababu hasa inaelezwa ni kubadili mbinu za soka ambazo amekataa kufanya huku akiamini mbinu zake za 4-4-2 ndio zitamsaidia zaidi lakini pia akiamini wachezaji aliowafundisha Napoli ndio wataweza kumsaidia ndio maana amemsajili Higuain.

Maurizio Sarri, kwa upande mwingine, anaamini wachezaji hawana msukumo nae wa kucheza na aliifanya kuwa taarifa kwa kuwa hawezi kuwahamasisha wachezaji, ambayo inaweza kumaanisha anaweza kuacha kuifundisha timu hiyo.

Hizo ndio sababu zinazoelezwa zilimsukuma Muitaliano huyo kusafiri tofauti na timu baada ya kupokea kipigo hicho kutoka kwa Bournemouth cha goli 4-0.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents