Burudani

Sababu ya Lulu Diva kuwakubali Jide, Vanessa, Beyonce na Celine Dion

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka kuhusu mastaa wa kike wa Bongo na wa nje anaowakubali.

Hitmaker huyo wa wimbo ‘Usimuache’, amesema kwa hapa Bongo anawatazama zaidi Lady Jaydee na Vanessa Mdee kwa namna wanavyofanya kazi zao kitu ambacho kinamuhamasisha na yeye kufanya hivyo.

“Kimataifa namuangalia sana Beyonce na Celine Dion. Nikimuangali Beyonce naangalia hadi life style yake anayoishi, nikimuangalia Celine namuangalia hata the way anavyoimba, anavyoweza ku-control sauti yake,” Lulu Diva ameiambia E FM na kuongeza.

“Beyonce kuanzia swagger anavyoimba, anavyocheza jukwaani, anavyocheza mwenyewe kwenye video zake, mavazi hata life style yake akiimba nakubali sana,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents