Siasa

Sababu ya Mbowe kuitwa Polisi yatajwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene, kimesema kuwa Jeshi la Polisi Kinondoni lilimuita Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ili kujua alikuwa anataka kuhutubia kitu gani kwa umma.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene, na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Makene ameyabainisha hayo leo Mei 15, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kueleza kuwa baada ya kumhoji kwa muda, hatimaye Jeshi hilo ilipofika majira ya jioni lilimuachia na kuruhusu aendelee na shughuli zake.

“Aliripoti akama ambavyo alipokea wito kutoka kwa RPC Kinondoni, na walitaka kujua sababu ya yeye kutaka kuzungumza na umma na baadaye jioni aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake, na suala la mkutano liko pale pale, kwahiyo sasa tunaangalia kwenye hotuba kama kutakuwa na vitu vya kubadilisha ama vibaki vile vile kulingana na wakati na siku” amesema Makene.

Jana Mei 14, 2020, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, ilikuwa azungumze na umma mubashara, lakini mkutano wake uliahirishwa baada ya kupokea wito wa Jeshi la Polisi Kinondoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents